katika uchaguzi wa Viongozi wa juu wa TAG unaoendelea mkoani Dodoma hivi sasa matokeo yaliopatikana kwa wakati huu ni kwamba Dk. Barnabas Mtokambali ambaye aliyekuwa ameshika kiti hiko kwa muda wa miaka minne aibuka tena kidedea kwa asilimia 93.
Ushindi huo ambao ameupata mara baada ya wachungaji 20119 kuandika majina ya anayestahili kugombea nafasi hiyo ili aweze kupigigiwa kura ambapo kabla haijafika katika mchakato huo wa kura hatimaye aliibuka kidedea kutokana na jina lake kurudia mara 1969 ambapo ni sawa na asilimia 93.
Awali kabla ya mchakato huo kuanza Askofu Dk. Mtokambali alitoa hotuba kali ya wachungaji kuacha kuenenda ki binadamu na kwamba waache kupiga kampeni na kutoa, kupokea Rushwa.
Pia katika uchaguzi huo hatua inayofuata ni nafasi ya Makamu Askofu pamoja na Katibu Mkuu.
No comments:
Post a Comment