KAMA ilivyokuwa kwa Askofu Mkuu Dk. Barnabas Mtokambali kurudi kwenye nafasi yake ndivyo ilivyokuwa kwa Makamu Askofu Dk.Magnius Muhiche japokuwa hali ilikuwa tete kwa upande wake kutokana na uchaguzi kurudiwa zaidi ya mara nne kwa ajili ya upinzani uliokuwepo baina yake na mgombea mwenza Askofu Lawrance Kametta.
Ushindi huo wa Dk. Muhiche, ambao aliupata kwa kura 1398 ulikuwa na mvutano mkubwa kutokana na kwamba halikuwa hafiki zaidi ya theruthi tatu japokuwa alikuwa akimpita kwa mbali mgombea mwenza jambo lililosababisha uchaguzi kurudiwa zaidi ya mara nne.
Wachungaji wapatao elfu tatu wako mkoani Dodoma kwa ajili ya uchaguzi lakini waliokuwa na sifa za kupiga kura ni elfu mbili mia moja na kumi na moja.
No comments:
Post a Comment