• KUPATA KITABU WASILIANA NA SINGO E MGONJA 0718422414

    Kuna mawakala wengi Walio wekwa Tanzania Nzima, Piga Imus hiyo hapo juu Utaelekezwa namna ya kupata kitabu chako.
  • KUPATA KITABU WASILIANA NA SINGO E MGONJA 0718422414

    Kuna mawakala wengi Walio wekwa Tanzania Nzima, Piga Imus hiyo hapo juu Utaelekezwa namna ya kupata kitabu chako

Tembelea site zingine


Monday, August 13, 2012

Ukijibu maswali haya utapata zawadi

Jiandae kujibu maswali makuu yanayohusu wokovu ambayo yamekuwa yakiwatesa hata baadhi ya wanatheolojia. zipo zawadi za vocha za Simu kwa ajili ya kuwatia moyo wale watakaofanya vyema. maswali haya yatakuwepo kwenye Blogs kesho jioni.

Wednesday, August 8, 2012

Dk.Muhiche aendelee kung'aa TAG

KAMA ilivyokuwa kwa Askofu Mkuu Dk. Barnabas Mtokambali kurudi kwenye nafasi yake ndivyo ilivyokuwa kwa Makamu Askofu Dk.Magnius Muhiche japokuwa hali ilikuwa tete kwa upande wake kutokana na uchaguzi kurudiwa zaidi ya mara nne kwa ajili ya upinzani uliokuwepo baina yake na mgombea mwenza Askofu Lawrance Kametta.

Ushindi huo wa Dk. Muhiche, ambao aliupata kwa kura 1398 ulikuwa na mvutano mkubwa kutokana na kwamba halikuwa hafiki zaidi ya theruthi tatu japokuwa alikuwa akimpita kwa mbali mgombea mwenza jambo lililosababisha uchaguzi kurudiwa zaidi ya mara nne.

Wachungaji wapatao elfu tatu wako mkoani Dodoma kwa ajili ya uchaguzi lakini waliokuwa na sifa za kupiga kura ni elfu mbili mia moja na kumi na moja.

Mtokambali Arudi kwa kishindo

katika uchaguzi wa Viongozi wa juu wa TAG unaoendelea mkoani Dodoma hivi sasa matokeo yaliopatikana kwa wakati huu ni kwamba Dk. Barnabas Mtokambali ambaye aliyekuwa ameshika kiti hiko kwa muda wa miaka minne aibuka tena kidedea kwa asilimia 93.

Ushindi huo ambao ameupata mara baada ya wachungaji 20119 kuandika majina ya anayestahili kugombea nafasi hiyo ili aweze kupigigiwa kura ambapo kabla haijafika katika mchakato huo wa kura hatimaye aliibuka kidedea kutokana na jina lake kurudia mara 1969 ambapo ni sawa na asilimia 93.

Awali kabla ya mchakato huo kuanza Askofu Dk. Mtokambali alitoa hotuba kali ya wachungaji kuacha kuenenda ki binadamu na kwamba waache kupiga kampeni na kutoa, kupokea Rushwa.

Pia katika uchaguzi huo hatua inayofuata ni nafasi ya Makamu Askofu pamoja na Katibu Mkuu.