WIKI jana tulikuletea sehemu ya kwanza ya ushuhuda wa Bw. Renatus Mungai, aliyesomeshwa katika hekalu la Freemasons la Nairobi, akalitumikia kwa miaka kadhaa, lakini pia akatoa kafara watoto wake watatu na sasa anajuta akiwa amekimbilia Tanzania. Anasema kuwa visa vyake na kundi hili ndivyo vilivyochangia Rais wa zamani wa Kenya Dainel Moi, kuunda tume maalumu ya kuchunguza waabudu shetani, ambayo ilihoji hadi maofisa kadhaa kutoka Tanzania. Leo katika sehemu ya pili, anaeleza jinsi alivyomfichia mkewe siri kubwa kuhusu vifo vya wanae, aliowatoa kafara kama ishara ya mapenzi yake kwa shetani.
“Niseme tu ukweli kuwa, tangu nilipooa na kupata mtoto wangu wa kwanza, nilianza safari nyingi za kiutumishi hekaluni, kutokana na elimu yangu na imani ambayo uongozi wa hekalu ulikuwa nayo kwangu, nilisafiri sehemu mbali mbali kutumika. Niliamini kuwa nastarehe hapa duniani kwa kuwa nikifa ndio utakuwa mwisho wa maisha yangu.
Habari kwamba kuna maisha baada ya kifo na hata hukumu kutokana matendo ya kila mtu, hiyo ilifutwa kichwani mwangu kule London, ambapo nilijifunza kwa umakini sana falsafa nyingine za ulimwengu wa kimaumbile na kwa kwamba, mifumo mingi ya dini ni hadithi zilizoandaliwa na watu wenye akili ili kuifanya dunia itawalike.
Kwamba maisha ya mwanadamu yanategemea mifumo ya kimaumbile, ambayo mwanadamu hawezi kuibadili kwa namna yoyote ile, hilo ndilo lililokuwa wazo kuu katika imani yangu.
Kwa kweli baba yangu alikuwa rafiki yangu sana, na siri nyingi za hekalu alinishirikisha mimi kuliko hata bibi, wakati fulani alijitolea nyumba yake kubomolewa na kiwanja chake kilichokuwa Mombasa, kijengwe hekalu jipya huko na aliniambia kuwa kujitoa kwake huko ndio njia bora zaidi ya kudhihirisha uaminifu kwenye hekalu.
Hata hivyo nilipata jaribu moja kubwa, ambalo lilikuwa ni kumficha mke wangu kuwa, mimi nilikabidhiwa na babu yangu hekaluni tangu utoto wangu na nimesomeshwa na hekalu na natumikia hekalu.
Nilimwambia kuwa mimi ni mtakwimu katika ofisi ya M&T, ya Nairobi ambayo ni miongoni mwa makampuni makubwa yenye Ofisi kubwa kati kati ya jiji la Nirobi. Huo ulikuwa ni uongo unaofanana sana na ukweli na kwa kweli usingeweza kujua siri iliyofichika nyuma ya pazia.
Ukweli ni kwamba, mimi nilikuwa nimeajiriwa na hekalu, lakini hekalu linamiliki vitega uchumi vingine tu ambayo vimesajiliwa kama makampuni ya watu binafsi na M&T ni sehemu ya makampuni hayo na mimi pale nilikuwa na Ofisi tu ingawa shughuli zote zilikuwa ni za hekalu hilo.
Mkewangu alikuwa ni muumini mwaminifu wa Kanisa la Lutherani na mara kwa mara alikuwa akinialika kuhudhuria ibada pamoja naye, ingawa mara kadhaa nilikuwa nakataa. Karibu kila siku alikuwa akiniuliza nasali wapi na kwanini siendi kanisani? Lakini nilikuwa nikimjibu bila kueleza msimamo wangu. Ugumu ulikuwa pale tulipopata mtoto wetu wa kwanza ambaye nilimuita kwa jina la Andy kwa heshima ya mlezi wangu mmoja katika hekalu, ambaye alinisaidia sana.
Nakumbuka baada ya mtoto wangu kuzaliwa, niliwaambia mabosi wangu habari hizo na walinipa zawadi nyingi sana, pamoja na pesa kiasi ambacho kilimshtua sana mke wangu. Nilipewa pia likizo ya miezi miwili ili nimsaidie mkewangu kumlea mtoto huyo mchanga. Ulikuwa ni ukarimu ambao kwa kweli ulimshangaza pia hata mama mtoto wangu.
Baada ya wiki kadhaa mke wangu aliniambia kuwa, inatupasa tujiandae kumpeleka mtoto kanisani akabatizwe, kama ilivyo kawaida ya waumini wa kanisa la Kilutheri, hata hivyo nilisita kwa kuwa mimi nilikuwa siamini kuhusu imani ya kanisa hilo na sikuwa tayari kwenda.
Nilikumbuka kiapo changu cha uaminifu nilichopewa kabla ya kupelekwa Londoni kusoma, kweli ilikuwa mtihani kwangu, kuamua na mwisho niliamua kumuuliza master, ikiwa kuna tatizo kwa mtoto kwenda Lutherani na mama yake peke yao, au mimi pia kuwasindikiza?
Nilimfuata babu nikamuomba ushauria, lakini alinionya kuwa, mimi ni mtoto wa hekalu niliyetolewa tangu utoto wangu, kwa hiyo sina mamlaka ya kufanya maamuzi magumu kiasi hicho bila kupata ruhusu tena ya maandishi kutoka kwa master.
Kwa kawaida wakati ule master alikuwa hakai Kenya, alikuwa akiishi Tanzania, hivyo nililazimika kusafiri hadi jijini Dar es Salaamu kuonana naye ili kuzungumzia suala hilo. Sikuwa na shaka kwa kuwa master tunaelewana naye sana na mara nyingi alinisaidia mambo makubwa na magumu sana, hata nilipokuwa Londoni mimi ndio nilikuwa ni kipokea fedha za kodi ya nyumba zake na kupeleka benki.
Nilikutana naye kwenye moja ya Ofisi zake kule Vingunguti na kuzungumza kwa muda mrefu, aliniambia kuwa, nifanye nifanyavyo nihakikishe kuwa mtoto huyo anafika kwanza hekaluni, kwa kuwa mimi ni mtoto wa hekaluni na baada ya hapo anaweza kwenda kwenye dini yoyote ile atakayo mama yake, kwa kuwa yeye hajui.
Kwa kweli huo ndio uliokuwa mtihani wangu wa kwanza, nikifikiria nitamchukuaje mtoto bila mama yake kujua? Baba aliniambia nimwambie mke wangu kuwa, tupokezane kumpeleka mtoto klini, ili na mimi nizoee zoezi hilo bila hata yeye kujua, ili nitakapoenda kiliniki niunganishe safari.
Nilipofikiria niliona hiyo ndiyo iliyokuwa njia sahihi, lakini nikajiuliza atakubali? Na hata akikubhali! si atataka mwezi wa kiwanza aende yeye au twende wote? Nilipozingatia hilo nilibaini kuwa, hata njia hiyo nayo haitafanikiwa . Nilimshirikisha rafiki yangu mmoja ambaye niliamini kuwa yeye ni “Mastermind” ambaye pia ni mtu wa hekalu aliyekuwa ametolewa huko na wazazi wake akiwa mdogo na alikuwa na akili sana.
Rafiki yangu huyo wa zamani ambaye kwa sasa ni miongoni mwa wanasiasa wanaotingisha siasa za Kenya, tena akipewa nafasi kubwa ya kugombea urais kwenye uchaguzi ujao, alitengua kitendawili hiki kwa sekunde tu, yeye alikuwa mekiwisha tengeneza mpango makini uliofanikisha kila kitu………..
Itaendelea
Kima cha chini cha mishahara moto mkali
WIKI iliyopita Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Managementi ya Utumishi wa Umma, Bi.Hawa Ghasia, alitangaza bungeni juu ya kupanda kwa mishahara kwa asilimia 40.2, huku akichanganua kuwa wataajiri watumishi zaidi ya 60 elfu ikiwa ni pamoja na kupandisha vyeo watumishi takribani 80,050 ambapo hata hivyo hakuweka wazi juu ya kima cha chini na cha juu cha mshahara,hali inayozua sintofahamu.
Wakiongea na Jibu la Maisha, wadau mbalimbali juu ya suala hilo, walisema kwamba, ikiwa serikali imekuwa ya kwanza kuwataka watumishi wake; wakiwemo Wabunge kutaja mali walizonazo bila kificho chochote, ni dhahiri kuwa walipaswa kutokuwa na kificho juu ya ongezeko la mishahara kwa wafanyakazi wake.
Mwanaharakati mmoja wa haki za binadamu ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini alisema kwamba, kutotangaza kiwango cha kima cha chini na cha juu mishahara na kutaja tu kwamba bajeti ni trillion 3.2 ni ukiukwaji wa haki, kutokana kwamba nyakati hizi ni za ukweli na uwazi, kama ambavyo Hayati Mwalimu Nyerere alikuwa akifanya.
“Kwa nini waogope kutaja, kama kweli ni kiwango kinachokidhi mfumuko wa bei kwa nini iwe kificho, inaonekana ni kiwango kidogo sana kimewekwa ndio maana wanapata kigugumizi, sasa watajuaje kama wanapunjwa; kutosema ni kuficha uovu,” alisema na kuongeza:
“Hii ndio maana viongozi wengine wanashindwa kutangaza mali walizo nazo, jambo ambalo si uadilifu, kwamba mishahara imepanda ni siasa tu kwa namna moja au nyingine inaweza kuleta mafarakano katika ndoa.”
Askofu wa Jimbo la Mashariki wa kanisa la TAG, Lawrence Kametta akitoa maoni yake alisema kwamba, hata kama kiwango cha mishahara kitapanda kama Waziri wa nchi ofisi ya rais management ya utumishi wa umma, Hawa Ghasia alivyosema, lakini serikali bado ina wajibu wa kufunga mianya ya mfumuko wa bei kwani, kwa kima cha chini bado hakitaweza kumfanya mtu kuishi bila kukuna kichwa.
“Mtu ukimpandishia mshahara kutoka laki moja mpaka laki moja na nusu, kama gharama za maisha ziko juu ni wazi kuwa, hazitaweza kumsaidia kitu,” alisema Askofu Kametta na akaongeza:
“Hapo awali serikali ilitangaza kuwalipa walimu malimbikizo ya madeni yao pamoja na kuongeza mshahara lakini mwisho wa siku haikufanya hivyo mpaka walimu wakaitisha mgomo, pia kutotaja kiwango halisi ni unyonyaji, mara nyingi imekuwa maarufu sana kutamka lakini utekelezaji ni duni.”
Naye daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake, Profesa Malise Kaisi akiongea na Jibu la Maisha alisema kuwa, serikali kushindwa kusema hadharani kuwa kima cha chini na juu ni shilingi ngapi kwa sasa sio kitu, isipokuwa watu wasubiri hadi pale watakapoanza kupewa hilo ongezeko na ndipo waweze kutoa maoni yao.
Mimi naona watu wangeipa serikali muda, wasubiri hadi watakapopewa hilo ongezeko na hapo ndipo watajua kwamba linakidhi mahitaji au la,” alisema Profesa huyo mkazi wa jijini Dar es Salaam.
Mchungaji Bruno Mwakibolwa wa Kanisa la EAGT, Mito ya Baraka la jijini Dar es Salaam, kwa upande wake alikuwa na haya ya kusema: “Serikali nayo ni mwanadamu, hivyo kwa namna moja au nyingine ina mapungufu na inaweza kukosea, hivyo katika hilo la mishahara pia tunapaswa kuwaombea kama tunavyoomba katika mambo mengine.”
Sambamba na hilo alisema, watu wengi huwa ni wepesi wa kulaumu, ambapo aliongeza kwamba Biblia inakataza kulaumu kwani; mtu wa jinsi hiyo mwisho wa siku naye huja kulaumiwa.
Wiki iliyopita Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais management ya utumishi wa umma, Hawa Ghasia alipokuwa akiwasilisha bajeti yake bungeni alishindwa kutangaza nyongeza ya mishahara ya watumishi wa Umma, ingawa kupitia Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo iliahidiwa kufanya hivyo, hata hivyo serikali ilisema itatumia shilingi trillion 3.2 katika mwaka huu wa fedha, huku ikisema kuwa, mishahara imeongezeka kwa asilimia 40.2.
Mchungaji afungwa jela kwa kuombea mgonjwa
MCHUNGAJI Yerzhan Ushanov, anayemtumikia Mungu katika kanisa la New Life Protestant la jijini Taraz, nchini Kazakhstan, amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela kwa kosa la kumwombea mgonjwa kwa jina la Yesu akapokea uponyaji na kuwa mzima.
Mashtaka ya Mchungaji huyo inaelezwa kuwa ni ya kutungwa kama yale aliyoshtakiwa nayo mtangulizi wa imani yake, yaani Bwana Yesu Kristo Mbele Ya Baraza la Sanhedrin na kuhukumiwa adhabu ya kusulubiwa hadi kufa.
Walioshuhudia mkasa huo uliotokea katika mji wa Taraz,nchini Kazakhstan, walisema kuwa Mchungaji Ushanov,ambaye amekuwa akiendesha huduma ya maombezi kwa makundi na kwa mtu mmoja mmoja alitegwa na polisi wa kikosi cha siri chenye jukumu la kukabiliana na Ukristo nchini humo (KNB)ili kipate sababu za kumshtaki.
Katika mashtaka yao KNB, wanadai kuwa Mchungaji Ushanov, alimzuru mtu mmoja ambaye alimuombea kwa jina la Yesu jambo ambalo ni kosa kwa kuwa maombi hayo yalimdhalilisha mumewe